Ufunguzi wa semina tatu za Quráni kwa wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza ufunguzi wa semina tatu za Quráni kwa wasichana wenye umri tofauti, chini ya usimamizi wa wasomi bobezi wa Quráni.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema kuwa: “Semina hizi ni sehemu ya kutimiza mkakati wa Maahadi katika harakati zinazo husu Quráni tukufu, ikiwa ni pamoja na sekta ya semina, semina hizi ndio harakati ya kwanza inayohusu Quráni kufanywa baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa: “Semina zimepangwa kulingana na umri wa washiriki, semina ya kikosi cha Alyaafiaat inahusisha wasichana wenye umri wa miaka (12 – 17), na semina ya Alhaamidaat, inahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu, huku semina ya (tutakusomesha hautasahau) inahusisha wanawake wenye umri mkubwa”.

Akasisitiza kuwa: “Semina zitaendeshwa ndani ya ofisi za Maahadi katika mkoa wa Najafu, tutafuata masharti yote ya kujikinga na maambukizi katika semina hizo, hata washiriki wamewekwa idadi maalum kwa ajili ya kuhakikisha umbali wa ukaaji kati ya mtu na mtu”.

Akamaliza kwa kusema: “Pamoja na semina hizi, Maahadi bado inasemina zingine ambazo inaendesha kwa njia ya mtandao, zinazo husu mada tofauti za Quráni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: