Kuanza kwa hatua ya pili ya semina ya (kujenga uwezo wa kiidara)

Maoni katika picha
Siku ya Alkhamisi ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), imeanza hatua ya pili ya semina ya (kujenga uwezo wa kiidara) chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wake.

Hatua ya pili ni maalum kwa ajili ya wasaidizi wa marais wa vitengo, wakati hatua ya kwanza ililenga marais wa vitengo na taasisi za Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tumeongea na rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Hassan Jaabir kuhusu semina hiyo, amesema kuwa: “Katika kufanyia kazi mtazamo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinaendesha semina za kuwajendea uwezo viongozi wa Ataba tukufu, baada ya kumaliza semina ya marais wa vitengo vyake”. Akaongeza kuwa: “Semina hii inalenga kujenga uwezo wa watengaji wa idara na wasaidizi wa marais wa vitengo”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba ya semina hii inahusisha makundi matatu, inatarajiwa kuchukua mwezi mzima, itakuwa na kipendele cha mafunzo kwa vitendo”.

Mjumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amesema: “Semina iliyopita ilihusisha marais wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu na ilidumu kwa muda wa miezi mitatu, na semina hii ni maalum kwa wasaidizi wa marais wa vitengo”.

Akaendelea kusema: “Mafunzo husaidia taasisi au ofisi husika kufanya kazi vizuri, hakika semina zinauzuri wake, ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kuwakusanya pamoja viongozi wote wa Ataba tukufu, jambo linalo saidia kubadilishana uzowefu baina yao, na kupata nafasi ya kila mmoja kueleza uzowefu wake kwa mwenzake”.

Akasema kuwa: “Semina hizi zimepata muitikio mkubwa sana, bado zitaendelea kwa watumishi wengine pia, tunakusudia kufikia watumishi wote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: