Karbala na mawakibu zake wanakumbuka mshairi Husseini Mahadi Al-Umawiyyi (r.a)

Maoni katika picha
Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika mji mtukufu wa Karbala, wamefanya kongamano la kueleza historia ya msomaji wa mashairi ya Ahlulbait (a.s) marehemu Mahadi Al-Umawiyyi Alkarbalai (r.a) baada ya miongo miwili tangu alipo fariki.

Kongamano limefanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s).. kilele cha wasila) ndani ya Husseiniyya ya Aali Yaasin mjini Karbala, na kuhudhuriwa na ugeni kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, pamoja na wawakilishi wa mawakibu Husseiniyya kutoka mikoa tofauti, na washairi pamoja na wapenzi wake na familia yake.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, amezungumza katika hafla hiyo.

Akauambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumezungumza historia ya mshairi huyu ambaye beti zake zimebaki nasi hadi leo, ikiwemo kaswida yake isemayo (Sisi bila Hussein hatuna wasila, na dhambi ni nyingi yatosha, kesho zitakuwa kwetu ngome ya kutuzuwia.. haya ni maoni yetu sote) kaswida hii ni kielelezo cha ikhlasi ya mtu huyu, ameendelea kuwa mtu muhimu katika majlisi zote”.

Akasisitiza kuwa: “Kufanya kumbukumbu hii ni jambo dogo sana kulingana na heshima yake, alitumia umri wake wote katika kumhudumia Imamu Hussein (a.s) kwa njia ya mashairi, alifanya kila awezalo katika kutangaza sauti ya Imamu Hussein (a.s)”.

Kumbuka kuwa mshairi Al-Umawiyyi ni miongoni mwa washairi wakubwa, kila siku anakumbukwa hasa katika mwezi wa huzuni mwezi wa Muharam, alitunga mashairi mengi yaliyosomwa na watu mbalimbali wa zama zake, akiwemo marehemu bwana Mula Hamza Zaghiir na bwana Jaasim Kakawi na Mahfuudh Khatwatwa na marehemu Hussein Tariri (r.a), inasemekana kuwa Mula Hamza Zaghiir alipewa jina la mshairi wa Umawiyyi na kiongozi wa washairi bwana Kaadhim Mandhuur (r.a), baada ya kumuimbia kaswida isemayo (Baina ummi yaa Hussein Zainabu tarani).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: