Ugeni kutoka Maahadi ya Quráni tukufu umetembelea taasisi ya Ain na kusifu utendaji wa taasisi hiyo

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, umetembelea ofisi za taasisi ya kijamii ya Ain katika mji mkuu wa Bagdad, kwa ajili ya kuangalia utengaji wake na kufungua ushirikiano baina yao, aidha kuwataarifu kuwa Maahadi ipotayali kutoa msaada wowote wa kielimu kuhusu Quráni tukufu ili kusaidia taasisi hiyo kufikia malengo yake. Ugeni huo umeongozwa na rais wa Maahadi Shekh Jawadi Nasrawi pamoja na jopo la viongozi wa vituo vilivyo chini yake.

Nasrawi Ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara hii ni sehemu ya shughuli za kibinaadamu zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kundi la mayatima, tumefuatana na wasomaji wa Quráni tukufu kutoka Ataba takatifu, tumeangalia harakati mbalimbali zinazofanywa na taasisi ya Ain katika mambo tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Tumesikiliza maelezo kuhusu mradi wa (kituo cha nyota za Zaharaa) ambao ni moja ya miradi muhimu inayo fanywa na taasisi, unalenga kuwafundisha mayatima ujuzi utakao wasaidia katika maisha yao, na kuwapunguzia ukiwa walionao, aidha tumeangalia utendaji wa mfumo wa masanduku ya sadaka na namna yanavyo tumika”.

Nasrawi akasema: “Kazi inayofanywa na watumishi wa taasisi hii tukufu ni kazi kubwa inastahiki kupongezwa, wanafanya kazi nzito ya kuhudumikia mayatima na familia zao, kazi hii inawaweka karibu na radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu, bila shaka thawabu za kazi hii haziwezi kuelezeka, tunawaombea watumishi wote wa taasisi hii Mwenyezi Mungu awape nguvu na uthabiti”.

Kumbuka kuwa taasisi ya kijamii ya Ain ni taasisi inayotoa misaada ya kibinaadamu kwa watu wote, imejikita zaidi katika kusaidia mayatima wa mashahidi miongoni mwa wapiganaji wa kujitolea, walio itikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kuilinda Iraq na maeneo matakatifu, pamoja na mayatima wa watu waliouwawa na mashambulizi ya magaidi hapa Iraq, na mayatima ambao wazazi wao wamekufa vifo vya kawaida wanao hitaji usimamizi, taasisi inapata msaada kutoka kwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: