Kituo cha miradi ya Quráni kinafanya vikao vya usomaji wa Quráni kila wiki ndani ya Maqaamu ya Imamu Mahadi (a.f)

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu, kinafanya vikao vya usomaji wa Quráni kila wiki ndani ya Maqaamu ya Imamu Mahadi (a.f) kwa ushiriki wa wasomaji wa Maahadi.

Vikao hivyo hufanywa kwa ushirikiano kati ya kituo na kitengo cha Magaamu ya Imamu Mahadi (a.f), kuanzia saa kumi na moja jioni kila siku ya Alkhamisi, na hurushwa mubashara na kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel pamoja na chanel ya Quráni tukufu ambayo ipo chini ya kituo cha luninga cha Karbala.

Tambua kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, hufanya vikao vya usomaji wa Quráni katika miji tofauti hapa nchini.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu pamoja na matawi yake ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha masomo ya Quráni, na kuchangia katika kutengeneza jamii inayofanyia kazi mafundisho ya Quráni na yenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika mambo mbalimbali yanayo husu Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: