Shindano la makala bora kuhusu bara la Afrika

Maoni katika picha
Kituo cha Dirasaat Afriqiyyah chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufanyika kwa shindano la Makala bora kuhusu bara la Afrika, kama sehemu ya kudumisha mawasiliano na bara hilo, na kuangazia maisha yake ya kawaida, Makala ihusu moja ya mada zifuatazo:

Kwanza: Dini.

Pili: Lugha na utamaduni.

Tatu: Siasa.

Nne: Uchumi.

Tano: Jamii.

Sita: Elimu.

Saba: Quráni.

Nane: Viongozi mashuhuri wa Afrika.

Masharti ya shindano:

 • - Makala isiwe na chini ya maneno (400) na yasizidi (1200), Makala itakayokua na chini ya kiwango cha maneno kilicho tajwa au zaidi haitakubaliwa.
 • - Iwe mpya ambayo haijawahi kuandikwa mahala popote.
 • - Mada iwe na uhusiano na bara la Afrika.
 • - Ikidhi vigezo vya kielimu.
 • - Isiwe imenakiliwa kutoka kwenye mitandao ya kijamii.
 • - Iandikwe kwa lugha fasaha ya kiarabu yenye kueleweka kwa urahisi na kujiepusha na makosa ya kilugha.
 • - Makala itokane na mada zilizo tajwa.
 • - Ijikite katika mada moja na ifafanue kwa ufupi.
 • - Iandikwe kwa kutumia program ya (word).
 • - Makala zitachujwa na jopo maalum la majaji.
 • - Makala zitumwe kwenye namba ya simu (07719889123) au kwa barua pepe katika anuani AFICANCENTER22@gmail.com

Tarehe ya mwisho kupokea Makala ni (20 Juni 2021m), tumeandaa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo pamoja na kutoa vyeti vya ushiriki, sambamba na kuandika Makala katika machapisho ya kituo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: