Wizara ya mipango: Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu imevuka jografia ya Karbala na imegawika katika sekta ya afya, elimu, utumishi na utamaduni

Maoni katika picha
Msemaji wa wizara ya mipango hapa Iraq, Ustadh Abdu-Zuhura Indawi amesema kuwa, Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu imevuka jografia ya Karbala, na imegawika katika afya, elimu, utumishi na utamaduni.

Yamesemwa hayo katika ziara iliyofanywa na Dokta Khalidi Batali waziri wa mipango, asubuhi ya Jumamosi katika Atabatu Abbasiyya na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria pamoja na katibu mkuu na makamo wake, na wajumbe wa kamati ya uongozi na marais wa vitengo vyake.

Handawi akasema: “Lengo la ziara hii ni kuangalia miradi inayofanywa katika mkoa wa Karbala, pamoja na miradi ya Atabatu Abbasiyya, ambayo inastahiki pongezi kwani imechangia upatikanaji wa ajira kwa kiwango kikubwa, na inafaa kusaidiwa.

Akasisitiza kuwa: “Tutasaidia juhudi za Ataba tukufu katika utekelezaji wa miradi hiyo, kwa sababu inatumikia wananchi pia ni msaada mkubwa kwa serikali katika kuiwezesha kutekeleza majukumu yake, Ataba tukufu zimekuwa nguzo muhimu za kuleta maendeleo katika taifa”.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar akasema: “Leo tumekutana na Mheshimiwa waziri wa mipango, na tumezungumza kuhusu huduma anazopaswa kupata mtu anaekuja kutembelea Ataba mbili takatifu, ambazo hutembelewa na mamilioni ya watu”. Akasema: “Watu hao wanahitaji kuhudumiwa, imma wahudumiwe na serikali au na Ataba zenyewe”.

Akaendelea kusema: “Mheshimiwa waziri tumemuonyesha mtazamo wa Atabatu Abbasiyya na miradi yake, pamoja na mikakati ya kiuchumi na matarajio yetu, ameshukuru na kupongeza kazi zinazo fanywa na Ataba ikiwa ni pamoja na kuendeleza raia wa Iraq hususan katika sekta ya elimu”.

Naye Mheshimiwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ashiqar akamshukuru waziri kwa ushirikiano mzuri anaotoa katika miradi ya Ataba tukufu.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh akasema: “Tunaushirikiano wa kudumu na wizara ya mipango, miradi yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo kamilika kwa wakati inatokana na ushirikiano wa wizara hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: