Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya harakati za kitamaduni katika mji wa Sanjaari

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa ratiba ya program ya kidini na kitamaduni ya kila wiki katika wilaya ya Sanjaari magharibi ya mkoa wa Mosul.

Chini ya usimamizi wa kituo cha utamaduni maelekezo na maendeleo, na kwa kushirikiana na mazaru ya bibi Zainabu Sughra iliyopo kwenye wilaya hiyo.

Msimamizi wa harakati hiyo Shekh Haidari Aaridhwi kutoka kitengo cha Dini ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Program hii ni miongoni mwa harakati za kituo katika wilaya, hufanywa kila wiki katika mazaru ya bibi Zainabu Sughura (a.s), asubuhi ya kila Ijumaa na kuhudhuriwa na wakazi wa mji wa Sanjaari.

Akaongeza kuwa: “Harakati inahusu usomaji wa Quráni na dua ya Nudba, kisha huswaliwa swala ya Ijumaa halafu hutolewa mawaidha yenye mafunzo elekezi ya kimalezi, kitabia, kifiqhi na mada zingine, halafu huzungumzwa moja ya tukio la kidini kwa undani”.

Kumbuka kuwa kituo hakihusiani na kundi la watu maalum, bali kinalenga makundi ya watu wote waliopo katika wilaya ya Sanjaari, Sunni, Shia, Turkumaan, Aizidiyyiin na Wakurdi, kinafanya shughuli nyingi, miongoni mwa shughuli hizo ni kutoa mihadhara, kufanya vikao vya usomaji wa Quráni pamoja na kufanya semina za kujenga uwezo, na miradi mingine inayo lenga kuwanufaisha wakazi wa Sanjaari, baada ya kupitia mateso makubwa wakati wa uvamizi wa magaidi wa Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: