Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imepata nafasi kumi kwenye mashindano ya Quráni ya kitaifa

Maoni katika picha
Mahafidh kumi kutoka Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamepata nafasi ya kushiriki kwenye shindano la kuhifadhi Quráni linalo simamiwa na idara ya malezi ya Iraq.

Washiriki hao wameandaliwa na idara ya Maahadi, na walishiriki mwenye mashindano ya awali (ya kuhifadhi na usomaji) yaliyofanywa katika mkoa wa Najafu na wakafanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Maahadi ya Quráni tawi la wanawake limesema: kupata idadi hiyo kubwa ya washiriki kunatokana na juhudi kubwa ya viongozi wa kitengo hicho, pamoja na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao umeweka mazingira mazuri katika kila sekta ili kurahisisha mfumo wa kuhifadhi Quráni, mafanikio mazuri yanayo onekana ni dalili ya kuwepo kwa utaratibu mzuri wa kuhifadhi Quráni.

Kumbuka kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake kupata nafasi za ushiriki, bali wamesha shiriki mara nyingi na kupata nafasi za juu, hii ni wazi kuwa Maahadi inamfumo mzuri wa kuhifadhisha Quráni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: