Jengo la Murtadhwa: Kilelel cha ujenzi bora wa Najafu na uzuri wa Abbasiyya

Maoni katika picha
Jengo la Murtadhwa (a.s) katika mkoa wa Najafu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni moja ya majengo bora katika mji wa kiongozi wa waumini (a.s).

Limejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (890) lina ghorofa saba, linatumiwa kwa ofisi za:

  • - Kituo cha kiislamu cha tafiti za kimkakati.
  • - Kituo cha tafiti za kiafrika.
  • - Kituo cha Shekh Tusi cha kuhuisha turathi.
  • - Kituo cha kukuza elimu na kuendeleza vipaji Alkafeel.
  • - Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya tafiti za kihauza kwa njia ya mtandao.
  • - Ukumbi wa kisasa wa mikutano, makongamano na nadwa.

Jengo hili jemejengwa na kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu katika mfumo wa kisasa kabisa, kuanzia umbo lake hadi umaliziaji wake na mifumo iliyowekwa, kama vile mfumo wa (wito, zimamoto, kamera, mawasiliano, gesi, vipaza sauti).

Jengo hili limejengwa ili kurahisisha utendaji wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya na matawi yake, vilivyo kuwa vinafanya kazi katika majengo yaliyokuwa hayaendani na shughuli zao, hivyo wamehamishiwa katika jengo ambalo linaendana na shughuli zao za sasa na za baadae, ndio maana Ataba ikaamua kujenga jengo maalum kwa ajili ya vituo hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: