Idara ya Quráni imetangaza tarehe mpya ya kuanza usomaji wa Quráni kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya tablighi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza tarehe mpya ya kuanza usomaji wa Quráni kwa njia ya mtandao.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema: “Tangazo hili linatokana na maombi yaliyo letwa kwenye kituo chetu ya kutaka tuendelea na ratiba ya usomaji wa Quráni kwa njia ya mtandao kama tulivyokuwa tukifanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa: “Idara ya Quráni itaanza ratiba ya usomaji kwa njia ya mtandao siku ya Jumanne ijayo tarehe (1/6/2021m) chini ya kauli mbiu isemayo (ili watafakari aya zake) saa (9:30) jioni, kupitia jukwaa la (google meet na telegram)”.

Akabainisha kuwa: “Kuna masharti ya kujiunga na program hii ya kila wiki, hairuhusiwi kutuma link ya kujiunga na program kwenye makundi ya mitandao ya kijamii, wanaume hawaruhusiwi kushiriki, mwisho wa kujiandisha ni saa 6 Adhuhuri ya siku ya ufunguzi”.

Akafafanua kuwa: “Kuna vipengele tofauti katika usomaji huo wa Quráni, kuna usomaji wa juzuu la Quráni kwa kupokezana, kuna visa vya mitume, maarifa ya Quráni, tafsiri na mengineyo”.

Akasema kuwa: “Muda ya ratiba hii ni saa moja na nusu, kwa kila anayependa kushiriki ajiandikishe kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/NycapDmLpGErBSGTA".
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: