Kukamilika kwa maandalizi ya kongamano la wanahabari awamu ya sita

Maoni katika picha
Idara ya jarida la Riraadhu Zaharaa (a.s)/ ofisi ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kukamilika kwa maandalizi ya kongamano, litakalo fanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (zoom cloud meeting) kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed na Alkafeel, chini ya kauli mbiu isemayo: (kutokana na mafundisho ya Fatuma Zaharaa (a.s) tunaongeza fikra zetu), siku ya Jumanne mwezi (19 Shawwal 1442h) sawa na (1 Juni 2021m) saa 9:00 jioni kwa saa za Bagdad.

Rais wa uhariri wa jarida bibi Laila Ibrahim Ramadhani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kongamano hili ni sehemu ya harakati zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya habari, hufanywa kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kuzinduliwa kwa jarida hili, huu ni mwaka wa (15) tangu kuanzishwa kwake, tunaangazia sekta ya habari kwa ujumla na kwa namna ya pekee habari zinazo husu wanawake, kwa ajili ya kuimarisha na kuitendea haki sekta hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Kawaida kongamano hili hufanywa kwa watu kuhudhuria moja kwa moja kutoka ndani na nje ya Iraq, lakini kutokana na uwepo wa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, kamati ya maamndalizi imeamua kufanya kwa njia ya mtandao, litakuwa na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni uwasilishaji wa mada tofauti za kitafiti”.

Kwa yeyote anayetaka kushiriki ajisajili kupitia link ifuatayo:

https://us02web.zoom.us/webinar/register/WN_fsHkH_wHRYa_INGJI8uSBg

Kumbuka kuwa jarida la Riyaadh Zaharaa (a.s) limejikita zaidi katika kuandika habari zinazo husu wanawake, zinazo endana na heshima ya mwanamke wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: