Muonekano wa malalo ya Nuur: Paa la haram tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Mradi wa upanuzi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa upauwaji wake, ni mwanzo wa historia mpya ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo faa kuandikwa kwa herufi za dhahabu, mradi huu unasehemu nyingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa paa la vioo.

Mradi huu umesanifiwa kwa namna ya pekee, unaendana na hadhi ya mwenye malalo hii takatifu (a.s), ujenzi huo umezingatia vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa paa (hema) za vioo zenye mambo makuu mawili:

  • Kila hema linawakilisha hema alizokuwa Abulfadhil Abbasi (a.s) anazisimamia katika vita ya Twafu.
  • Idadi ya hema hizo ni (34) inawakilisha umri aliokuwa nao Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu.

Mambo hayo mawili ndio yaliyotengenezewa muonekano huo.

Wasifu wa hema hizo ni:

  • - Idadi ya hema za vioo ni (34).
  • - Kila hema linauzito wa (tani 3.5).
  • - Vioo vilivyotumika kufunika hema hizo vinaukubwa wa (mt 6 x 6) na urefu wa (mt 1.5).
  • - Vioo vinatabaka tatu, vinaunene wa (sm 3.8) na uwezo wa (0.24).
  • - Vioo vya hema vimegawanyika sehemu tato, kukiwa na aina ya Jilatin, inayozuwia kuvunjika, pamoja na tabaka za kupambana na hewa.
  • - Tabaka la kioo cha juu linamadini ya kuzuwia vumbi (Nanotechnology), rangi yake inafanana na rangi ya mbingu, kwa ajili ya kupunguza miale ya jua hususan linapo akisi kuta na ardhi ya Ataba tukufu, na inasaidia kuongeza mwanga na uzuri wa sehemu.
  • - Vipande vya vioo ni rahisi kuvionganisha na vinauzito mdogo, vigumu kuvunjika, vinamuonekano mzuri, vinavumilia mazingira tofauti ya hewa, vinazuwia miale ya jua.
  • - Vioo vinauwezo mkubwa wa kuzuwia joto na sauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: