Kituo cha turathi za Karbala kimechapisha kitabu cha (muhtasari wa kitabu cha thawabu za vitendo).

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha kitabu cha (muhtasari wa kitabu cha thawabu za vitendo) cha Shekh Taqi-Dini Ibrahim bun Ali Kafámi Al-Aamiliy wa mwaka (823 – 905h).

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo cha turathi za Karbala Dokta Ihsani Gharifi: “Kitabu hicho kimetokana na uhakiki wa kituo cha turathi za Karbala na kinatokana na mihtasari ya Shekh Kafámiy katika nyaraka zake za (bustani ya nafsi na mapambo ya harusi) pamoja na mambo aliyo andika katika fani tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Chapisho la kitabu cha muhtasari wa kitabu cha (thawabu za vitendo) cha Shekh Swaduuq kilicho fanyiwa muhtasari na Kafámiy, bila kusema sababu zilizopelekea afanye muhtasari, muhtasari huu tunaweza kuueleza kwa ufupi kama ifuatavyo:

  • a- Kufuta mapokeo ya riwaya na kutosheka na kutaja jina la maasumu aliyepokea riwaya.
  • b- Kuchagua baadhi ya riwaya zinazo zungumzia maudhui moja, na kuacha zingine hatakama zinatofautiana madhumuni, idadi ya hadithi zilizo fupishwa imefika mia tatu na mbili (302) katika hadithi mia nane na tatu (803) zilizopo katika kitabu cha (thawabu za vitendo).
  • c- Imefupishwa orodha ya mapokezi ili kufupisha kitabu, na sehemu zingine orodha imeachwa kama kawaida.
  • d- Kufuta anuani za hadithi zilizo andikwa na Shekh Swaduuq”.

Kumbuka kuwa kitabu kinapatikana katika vituo vya mauzo vya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, karibu na mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: