Riyaadhu Zaharaa (a.s) imekhitimisha kongamano la habari

Maoni katika picha
Idara ya jarida la Riyaadhu Zaharaa (a.s) katika maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake, chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu alasiri ya leo siku ya Jumanne (19 Shawwal 1442h) sawa na tarehe (1 Juni 2021m) imekhitimisha shughuli za kongamano la habari kwa wanawake awamu ya sita, chini ya kauli mbiu isemayo: (kutoka katika mafundisho ya Fatuma Zaharaa (a.s) tunapata fikra zetu), limefanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (zoom), kwa ushiriki na ufuatiliaji wa wasomi wa sekula na waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya Iraq.

Bibi Laila Ibrahim Ramadhani rais wa wahariri wa jarida ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kongamano la mwaka huu limekua na upekee wake pamoja na kufanywa kwa njia ya mtandao, kamati ya elimu ilikuwa ya wanawake watupu tena waandishi wa jarida, haya ni mafanikio makubwa, aidha mada zilizo walisilishwa zitaandikwa katika jarida”.

Akaongeza kuwa: “Tukiwa kama wasimamizi wa kongamano hilo pamoja na ugumu wa mazingira tunayo pitia, kwa msaada wa Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa kitengo cha maktaba ya Ummul-Banina (a.s) tumefanikiwa kufikisha ujumbe wa kongamano, ni matumaini yetu kuwa tumefikia malengo”.

Akaashiria kuwa: “Tunatarajia kuona maendeleo zaidi mwaka kesho kutokana na mikakati ya jarida Insha-Allah, shukrani zimuendee kila aliyechangia kufanikiwa kwa kongamano hili la sita”.

Kumbuka kuwa kongamano limefana kutokana na kuhudhuriwa na walimu wa sekula, lilikuwa na mwitikio mkubwa uliolenga kuboresha sekta ya habari zinazo husu wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: