(Mashahidi wa Aqida) juzuu la sita limeandika historia ya makumi ya mashahidi

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha toleo la sita la kitabu cha (Mashahidi wa Aqida na taifa).

Juzuu hili limeandika historia ya mashahidi mia moja na sita (106) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, ili kuwa ukumbusho kwa waliopo na watakaokuja.

Kitabu hiki kinaandika historia ya mashahidi wa fatwa ya jihadi kifaya katika mji wa Basra, kimeandika orodha kubwa ya mashahidi watukufu, hususan mashahidi wa Hashdu-Shaabi wenyeji wa Basra, walio itika wito wa haki na wakaingia vitani kupigana na magaidi, wakapigana kwa moyo na Imani kubwa hadi wakapata shahada, na kuwa moyo wa historia baada ya roho zao kwenda kwa Mola wao, damu zao zikatoa maisha mapya kwa jamii na zimekuwa ni mwanga unao angazia wapitaji na kigezo chema kwa mujahidina.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Basra kinatoa machapisho mengi kuhusu turathi za Basra zinazo husu Dini, lugha na historia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: