Wataalamu wa kitengo cha uokozi Alkafeel wanaendelea na mafunzo ya kitabibu chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, mafunzo yamepewa jina la (katika kila nyumba kuna muokozi) yanayo husisha watumishi wa vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya ukumbi wa jengo la Shekh Kuleini.
Mkufunzi wa semina hiyo amesema kuwa: “Lengo la semina ni kuandaa watu wanaoweza kutoa huduma za awali kimatibabu katika jamii, watakao weza kusaidia kwa dharura”.
Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mafunzo muhimu yaliyo tolewa ni jinsi ya kuokoa mtu mwenye tatizo la moyo awe mzee au mtoto na namna ya kujikinga na maradhi ya kuambukiza”.
Akafafanua kuwa: “Ratiba inalenga kufundisha mbinu za kutunza uhai, chini ya mkakati wa kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanao toa huduma moja kwa moja kwa mazuwaru, ili waweze kutoa huduma sahihi na haraka kwa zaairu yeyote atakaepatwa na tatizo la afya”.
Akaendelea kusema: “Masomo yanatolewa kwa njia ya nadhariya na vitendo, wanashiriki watumishi (8) katika kila semina, ili kupata nafasi nzuri ya kuwafundisha kwa vitendo na kupima uwezo wao katika uokozi wa kitabibu”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi wake kwa lengo la kujenga uwezo wao na kukuza vipaji vyao.