Kuendelea na mradi wa mauwa ya Fatwimiyya

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na mradi wake uitwao (mauwa ya Fatwimiyya), unao husu wanafunzi wa kike waliofikisha miaka ya kubalekhe wanaosoma katika shule za Karbala, kwa kushirikiana na mkuu wa kituo cha malezi.

Mradi huu unatokana na jinsi Atabatu Abbasiyya tukufu inavyo lipa umuhimu kundi hili la vijana waliopo katika umri wa kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, kwa lengo la kuwajulisha wajibu wao kisheria katika uhusiano wao na Mola wao, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa swala, ibada ambayo humzuwia mja kufanya aina zote za maovu, na kuzingatia hijabu vazi ambalo huweka uhusiano mwema kati yake na jamii.

Makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika mradi huu unapewa kipaombele na kusaidiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, aidha umeitikiwa vizuri na idara za shule pamoja na wazazi na walezi wa watoto, umekuwa na mafanikio mazuri, matunda yake yameonekana katika awamu zilizo tangulia, leo tunafanya shughuli hii kwa kufuata masharti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kutangaza kuanza kwa mradi, tumepokea maombi kutoka idara za shule za mikoani, hadi sasa tunajumla ya maombi ya washiriki (3115) ambao ni mabinti wanaofikisha miaka ya kuwajibikiwa na sharia”.

Akafafanua kuwa: “Leo tumeanza kutekeleza mradi kwa kufuata ratiba maalum ya shughuli hii, tunatarajia kufanyia kazi maombi yeto yaliyotufikia, ratiba yetu inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni:

  • - Mhadhara kuhusu hijabu na umuhimu wake kwa mabinti.
  • - Usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na kutafsiri baadhi ya aya zinazo himiza hijabu.
  • - Historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuangalia hadithi zao pamoja na kuzilinganisha na mazingira halisi ya sasa.
  • - Masomo ya Fiqhi na Aqida yanayo endana na umri wao.
  • - Vipindi vya mapumziko na michezo mbalimbali.
  • - Kufundisha swala kwa usahihi.

Hali kadhalika tumewagawia nguo maalum za kuswalia, pamoja na zawadi za kutabaruku na Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kuwapa vitini vinavyo himiza hijabu, swala na ibada zingine kwa njia rahisi”.

Idara za shule na wazazi wa wanafunzi wamepongeza Atabatu Abbasiyya kwa kufanya shughuli hii tukufu inayo lenga wasichana wanao ingia katika umri wa kuwajibikiwa na sheria, kwa kuwajulisha mambo wanayo takiwa kufanya kulingana na umri wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: