Kituo cha kiislamu Alkafeel chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa: Bidhaa za shirika la Nuurul-Kafeel zinaubora mwingi, miongoni mwa ubora wake zimekamilisha masharti ya kisheria na kiafya, hivyo zinakubalika sana na raia wa Iraq.
Rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Swalahu Khafaji amesema kuwa: “Kituo kilianzishwa tangu lilipo anzishwa shirika la Nuurul-Kafeel, na kikaanza kuzalisha nyama nyeupe na nyekundu, kinafanya jambo muhimu sana ambalo ni kusimamia uchinjaji kwa mujibu wa sheria za kiislamu, kupitia kikosi kazi maalum kilicho bobea katika kazi hiyo na chenye uzowefu wa zaidi ya miaka kumi”.
Makamo rais wa kitengo hicho “Shekh Aadil Wakiil akaongeza kuwa: watumishi wa kituo cha Alkafeel wanasimamia uchinjaji wa wanyama tofauti kwa umakini wa hali ya juu, wanahakikisha yanatekelezwa masharti yote ya kisheria pamoja na taratibu zote za awali”.
Kumbuka kuwa “mradi wa nyama za Alkafeel huchija wanyama kwa kutumia mkono kwa kufuata sheria za Kiislamu, wanazalisha nyama salama kiafya na kisheria, kwa bei rahisi tofauti na nyama zinazo agizwa kutoka nje ya nchi, huku kiasi kikubwa hazujulikani vyanzo vyake wala mazingira ya kuchinjwa kwake, kituo hiki kipo chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo cha uchumi kinasimamia usambazaji wa nyama ndani na nje ya Iraq, pamoja na kusimamia bei na kuzuia aina yeyote ya udanganyifu (ghushi), wajumbe wa kitengo hicho wanapatikana katika machinjio zote, zinazo tumiwa na kituo hiki ndani na nje ya Iraq”.