Makamo katibu mkuu apongeza kazi zinazo fanywa na watumishi wa Maahadi Alkafeel ya watoto wanaoweza kujifunza

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussawi, amepongeza kazi zinazo fanywa na watumishi wa Maahadi Alkafeel ya watoto wanaoweza kujifundisha, kwa namna wanavyo wahudumia watoto hao na kuwafanya wajihisi vizuri pamoja na kuwaingiza katika jamii.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea Maahadi na kukutana na viongozi wa idara ya elimu, wamejadili utendaji kazi na changamoto wanazo weza kupata kama ofisi na namna ya kuzitatua, Maahadi hii inaidadi kubwa ya watoto wanaoweza kujifunza, ambao wanapewa huduma za malezi na elimu.

Hali kadhalika ameambiwa huduma zinazotolewa na Maahadi kwa watoto hao, ambazo zimesaidia kubadili tabia na kuwaimarisha kimasomo kwa kuwafundisha fani mbalimbali zinazo wawezesha kuwa watu bora katika jamii.

Makamo katibu mkuu amepongeza kazi zinazo fanywa na Maahadi, ya kutunza kundi hili muhimu la watoto, wenye baadhi ya changamoto za kiakili, akamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na uwezo wa kuendelea kuhudumia watu hawa na jamii kwa ujumla.

Kumbuka kuwa Maahadi inapokea watoto wenye tatizo la akili (wanaoweja kujifunza), wenye umri kati ya miaka (5 – 13) kwa wanaume na miaka (5 – 20) kwa wanawake, wenye matatizo ya akili (matahila) pamoja na wenye uzito wa kuongea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: