Mradi maji mbadala “Saaqi” ni sehemu ya kimkakati katika miradi ya utoaji wa huduma

Maoni katika picha
Mradi wa Saaqi unapewa kipaombele sana na Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi huu ni sehemu ya mkakati wa kupambana na ukame unaolikumba taifa la Iraq, hakika ni muhimu kuwa na miradi ya kupambana na janga hatari la ukame.

Kwa kuwa taifa linapitia matatizo mengi yamechangia kudhofika kwa idara ya maji, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaamua kufanya mradi huu katika ardhi ya mkoa mtukufu wa Karbala, kwenye jangwa la magharibi ya mji, mradi huu unasaidia kupunguza ukame na tatizo la maji.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Utekelezaji wa mradi huu ni muendelezo wa miradi ya utoaji wa huduma inayo fanywa katika mji mtukufu wa Karbala, na katika taifa la Iraq kwa ujumla”.

Akaongeza kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya mradi wa Saaqi wa maji mbadala baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu mradi huo, ulio ongozwa na taasisi ya maendeleo na mazingira ya Iraq na chuo kikuu cha Karbala pamoja na wizara ya maji tangu mwaka (2014), baada ya kujiridhisha ndio Atabatu Abbasiyya ikaanza utekelezaji wa mradi huo na kuhakikisha unatoa matunda tarajiwa ambayo ni maji ya kutosha kutoka aridhini”.

Akafafanua kuwa: “Mradi unahusisha visima (55) ambavyo vimeunganishwa kupitia mtandao wa mabomba yenye urefu wa kilometa (75), ukubwa wa eneo la mradi ni (dunam 10,000), hatua ya kwanza ya ujenzi ilianza mwaka 2016, kwa kuchimba visima (50) kila kisima kinauwezo wa kutoa maji lita (20) hadi (30) kwa sekunde, hivyo visima vyoto vinazalisha karibu lita (1500) kwa sekunde, tumeweka mfumo wa kudhibiti kufurika maji na kuyahifadhi kwa utaratibu mzuri, tumeandaa visima (3) maalum vya kutunzia maji kwa kushirikiana na wizara ya maji kwa ajili ya tafiti za kielimu”.

Akamaliza kwa kusema: “Maji yanayo zalishwa katika mradi huu baada ya kuyapima katika maabara, imethibiti kuwa yanauwezo mkubwa wa kutumika kwa shughuli za kilimo, na yanaweza kutumika kwa kunywa pia baada ya kuyasafisha, mitambo ya mradi huu inatumia umeme wa jua”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: