Watu wa Karbala wanampa pole Imamu Alkaadhim katika kumbukumbu ya kufiwa na baba yake (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa Karbala kupitia maukibu zao za kuomboleza, wametoa rambirambi na kumpa pole Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) kwenye malalo yake takatifu katika mji mtukufu wa Kadhimiyya, wakati wa kuomboleza kifo cha baba yake Imamu Jafari Swadiq (a.s), jioni ya Jumapili (24 Shawwal 1442h) sawa na tarehe (6 Juni 2021m) kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kiongozi wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kuhuisha kifo cha Imamu wa sita miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) mbele ya malalo ya mwanae Imamu Alkaadhim (a.s) ni utamaduni walio zowea watu wa Karbala toka zamani na wamerithi kutoka kwa babu zao”.

Akaongeza kuwa: “Waombolezaji wamefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya muombolezwa, baada ya kuwasili hapo kwa ajili ya maombolezo, majlisi imepambwa na kaswida pamoja na tenzi zilizo amsha hisia za huzuni ya msiba na kuwapa pole watu wa nyumba ya Mtume (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Ataba mbili tukufu imeandaa gari za ukubwa tofauti kwa ajili ya kubeba waombolezaji kutoka Karbala hadi Kadhimiyya”.

Kumbuka kuwa mawakibu hizi za waombolezaji hufanywa kila mwaka na wakazi wa mji wa Karbala, katika kuhuisha matukio ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), hushirikisha mawakibu na vikundi tofauti vya Husseiniyya katika mji mtukufu wa Karbala, pamoja na wakazi wa mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: