Ataba mbili tukufu zinapokea mawakibu za waombolezaji

Maoni katika picha
Katika kuhuisha kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s), tangu mapema asubuhi mawakibu za watu wa Karbala na maeneo jirani zimemiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kuja kutoa pole kwa msiba huu.

Mawakibu za kuomboleza huwasili mapema katika malalo hizo kwenye kila tukio la msiba wa Imamu (a.s), ukiwemo msiba huu wa kifo cha Imamu wa sita katika Maimamu wa Ahlulbait (a.s), huu ndio utamaduni wa uombolezaji uliozoweleka tangu zamani, kitengo cha utumishi katika malalo hizo mbili pamoja na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya huratibu matembezi yao.

Kumbuka kuwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu na kumpa pole Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) kwa kifo cha babu yake Swadiq (a.s), aliye uwawa na kiumbe muovu zaidi kwa dhulma, kwa kupewa sumu kali iliyosambaa ndani ya muili wa Imamu (a.s) hadi akafa, tarehe ishirini na tano Shawwal mwaka wa (148) hijiriyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: