Chuo kikuu cha Al-Ameed kinaomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaomboleza kifo cha Imamu wa sita Jafari Swadiq (a.s), kwa kufanya majlisi ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s) katika chuo hicho, na kuhudhuriwa na rais wa chuo na wasaidizi wake pamoja na viongozi wa vitengo, wakufunzi, watumishi na wanafunzi.

Majlisi imeandaliwa na kitengo cha maelekezo na malezi katika chuo hicho, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo, yakafuata mawaidha yaliyotolewa na Shekh Muhammad Kuraitwi kutoka kitengo cha Dini, akaeleza historia ya maisha na jihadi ya Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s), pamoja na elimu yake na hazina aliyo uachia umma wa kiislamu, na jinsi alivyo fungua chuo kikuu cha elimu mbalimbali ambacho walihitimu zaidi ya wanafunzi (4000), waliojaza elimu dunia nzima.

Hali kadhalika akaeleza utaratibu aliotumia Imamu katika kufundisha, akasisitiza kuwa tunatakiwa kujifunza kwake (a.s), namna alivyo fundisha utamaduni na elimu pamoja na mwenendo wa Ahlulbait (a.s) kama alivyo kuwa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), wanachuoni wakubwa walisoma kwake (a.s), akahitimisha mawaidha kwa kusoma utenzi ulio amsha hisia za huzuni, baada yake akapanda mimbari mmoja wa watumishi wa chuo na kusoma shairi la kuomboleza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: