Wataalamu wa Alkafeel kikosi cha uokoaji na mafunzo ya kitabibu chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, wanaendelea na semina za (muokozi katika kila nyumba) kwa watumishi wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya ukumbi wa jengo la Shekh Kuleini.
Tumeongea na rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema: “Wataalamu wa Alkafeel kikosi cha uokoaji na mafunzo ya kitabibu wanaendelea na ratiba ya semina za (muokozi katika kila nyumba), ratiba hii inamalengo mawili, kwanza kufundisha mbinu za uokozi katika kila nyumba ya muiraq. Pili kuwafundisha watumishi wa Ataba tukufu mbinu za uokozi, ili waweze kusaidia shughuli za uokozi iwapo likitokea tatizo lolote katika mazingira ya kazi zao hasa wakati wa ziara kubwa zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu hapa Karbala”.
Akaongeza kuwa: “Ratiba itaendelea ndani ya mwezi mzima kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa ziara ya Ashura, tunatarajia kutoa mafunzo haya kwa idadi kubwa ya watumishi, atakaye hitimu mafunzo haya atapata nafasi ya kushiriki katika uokozi wa kitabibu kitaifa”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya huwapa semina watumishi wake kwa ajili ya kuendeleza uwezo wao na kukuza vipaji vyao katika fani tofauti.