Waziri wa maji atembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Waziri wa maji Mhandisi Mahadi Rashidi Hamdani ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumatano baada ya Adhuhuri.

Alipo maliza kufanya ibada ya kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s), Mheshimiwa waziri amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqari na baadhi ya marais wa vitengo.

Katika ziara hii wamejadili mambo mbalimbali yanayo husu utoaji wa huduma kwa wananchi, hususan katika sekta ya maji na umwagiliaji, aidha wameongea kuhusu miradi ya kimkakati inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta hiyo muhimu.

Mwisho wa kikao chao katibu mkuu akampa mwaliko Mheshimiwa waziri wa kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayo husiana na wizara yake, Mheshimiwa kaonyesha kuwa yuko tayali kutoa ushirikiano katika hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: