Maktaba ya chuo kikuu cha Al-Ameed imezawadia maktaba ya chuo kikuu cha Nahrain mtambo wa kupuliza dawa kwenye vitabu

Maoni katika picha
Maktaba ya chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeizawadia maktaba ya chuo kikuu cha Nahrain mtambo wa kisasa unaopuliza dawa kwenye vitabu kwa kutumia mwanga.

Makamo kiongozi mkuu wa maktaba katika chuo kikuu cha Al-Ameed bibi Aliya Fadhili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Zawadi hiyo ni sehemu ya kukuza ushirikiano baina ya chuo chetu na vyuo vingine, hili sio tukio la kwanza, yapo matukio mengine yaliyofanyika siku za nyuma”.

Akaongeza kuwa: “Mtambo uliotolewa zawadi umetendenezwa na wataalamu wa chuo chetu, na umeonyesha mafanikio makubwa, unapuliza dawa kwenye vitabu na nyaraka za karatasi kwa kutumia mwanga, unauwezo mkubwa wa kuuwa bakteria na virusi ambayo huharibu vitabu vilivyo kaa muda mrefu pila kutumiwa, sambamba na kulinda usalama wa watumiaji wa vitabu hivyo na watumishi”.

Akabainisha kuwa: “Katika kuboresha uhusiano, maktaba ya chuo cha Nahrain imeahidi kuipa vitabu mbalimbali maktaba ya chuo kikuu cha Al-Ameed”.

Uongozi wa maktaba ya chuo kikuu cha Nahrain umeshukuru sana kwa kupewa zawadi hiyo tukufu, umeahidi kuendeleza ushirikiano baina yao kwa ajili ya kuboresha elimu katika taifa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: