Namna gani Atabatu Abbasiyya inasaidia kuboresha mazingira ya mji wa Karbala?

Maoni katika picha
Kutokana na siku ya kimataifa ya mazingira (WED) ambayo inasadifu tarehe tano ya mwezi huu, tunaangalia mchango wa Atabatu Abbasiyya katika swala hilo, kupitia sekta tofauti ikiwemo ya upandaji miti katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Hiyo ni sekta ambayo inasaidiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuongeza muonekano wa kijani kibichi katika mkoa wa Karbala, imefanya kazi kubwa kwa ajili ya kufanikisha swala hilo, miongani mwa kazi hizo ni kupanda miti kwenye barabara kuu na ndogo za hapa mkoani, miti imependezesha muonekano wa mji huu mtakatifu, na imechangia kuboresha mazingira.

Shamba boy wa Alkafeel ndio waliochukua jukumu la upandaji wa miti, kwa kutegemea uwezo wake binafsi, kupitia miche ya miti waliyonayo katika vitalu vyao, kazi hiyo imefanywa kwa awamu, walianza katika barabara kubwa na ndogo za mji mkongwe zilizopo karibu na zinazo elekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye barabara kuu.

Upandaji wa miti umefanywa kwa kufuata utaratibu maalum ambao haujaathiri majengo, aidha kazi hiyo haishii kwenye kupanda miti peke yake, bali kuna kikosi kingine kinahusika na umwagiliaji, uwekaji wa mbolea, uchambuliaji na ubadilishaji wa mji uliodhofika na kupanda mwingine, kazi hii hufanywa kila siku ndani ya mwaka mzima.

Miti iliyo pandwa pembeni ya barabara inamuonekano wa kijani na inauwezo mkubwa wa kuhimilia mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile miti ya Qarnaful, Akasiya, Surantis na mingineyo, ni miti mikubwa na inauwezo wa kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa mradi huo, miti hiyo imepandwa maelfu na imesaidia kuporesha mazingira, sambamba na muonekano mzuri wa miti hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: