Semina kuhusu fani za utangazaji wa redio kwa watumishi wa redio ya Alkafeel ya wanawake

Maoni katika picha
Redio Alkafeel ya mwanamke wa kiislamu chini ya kitengo cha elimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeendesha semina ya fani za utangazaji wa redio, watumishi wanao fanya kazi katika redio wameshiriki kwenye semina hiyo, inalenga kuwajengea uwezo katika kazi za kuendesha vipindi vya redia na usomaji wa habari, pamoja na fani ya kuandaa vipindi.

Mkufunzi wa semina ni Ustadh Adnani Alwani kutoka idara ya taaluma katika chuo kikuu cha Alkafeel, semina imedumu kwa muda wa siku tano, amefundisha namna ya kuendesha majadiliano na aina za mahojiano kwenye redio, pamoja na umuhimu wa vipindi vinavyogusa jamii kwa ajili ya kufikia malengo ya redio.

Akaeleza namna ya kuchagua watu wa kuwaalika kulingana na aina ya mada ya kipindi, na namna ya kutumia kipaji na uwezo wa mgeni aliyealikwa kwenye kipindi, uandaaji wa vipindi kwa kufuata misingi ya utangazaji, njia za majidiliano kulingana na mada husika, hali kadhalika amebainisha masharti ya lazima yanayo takiwa kuzingatiwa na muongozaji wa kipindi cha redio, ikiwa ni pamoja na uwelewa wa mada anayo jadili.

Kumbuka kuwa redio Alkafeel ya wanawake inatangaza mambo ya kidini, kijamii, kitamaduni na kimalezi, inavipindi vizuri vya kibunifu na mafundisho ya kiislamu sambamba na maadili ya kiiraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: