Maonyesho ya vitabu kimataifa katika mji wa Bagdad yamepambwa na machapisho mbalimbali ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa katika mji wa Bagdad awamu ya thelathini na mbili, yaliyo anza jana siku ya Alkhamini chini ya kauli mbiu isemayo (kitabu na taifa), washiriki ni zaidi ya taasisi (220) za usambazaji wa vitabu kutoka ndani na nje ya nchi.

Maonyesho haya yamehusisha aina za machapisho (130), ikiwa ni pamoja na vitabu vikubwa vyenye juzuu nyingi (mausuaat), vitabu tofauti, majarida yanayo andika mambo ya utamaduni yanayo chapishwa na vituo vilivyo chini ya kitengo hiki, kama vile (kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Basra, kituo cha turathi za Hilla, Maahadi ya Quráni tukufu), sambamba na mabango yanayo onyesha hati za kiarabu na mapambo ya kiislamu.

Kiongozi wa tawi linalo shiriki kwenye maonyesho haya Ustadh Mustwafa Abdusataar Shimri amesema kuwa: “Kitengo chetu kinashiriki kwenye maonyesho haya kwa kuzingatia kuwa ni sehemu ya harakati za kielimu na kitamaduni inayo lenga kuhuisha turathi za kiislamu”.

Akaongeza kuwa: “Upekee wa tawi letu ni kwamba vitabu vyote tunavyo onyesha vimeandikwa au kuhakikiwa na watumishi wa kitengo chetu, tunapenda kushiriki kwenye maonyesho ya aina hii na makongamano, kwa ajili ya kufikisha ujumbe wetu na machapisho yetu kwa idadi kubwa ya watu ndani ya muda mfupi”.

Tambua kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kimesha shiriki mara nyingi kwenye maonyesho tofauti ya kitaifa na kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: