Maahadi ya Quráni tukufu katika wilaya ya Hindiyya imekaribisha mradi wa (Mimbari za nuru)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya imekaribisha mradi wa (Mimbari za nuru), unaosimamiwa na kituo cha miradi ya Quráni na kushiriki kundi la wasomaji wa Quráni na washairi.

Wasomaji wa Quráni kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pia wameshiriki, pamoja na kundi la washairi kitoka kikosi cha waimbaji cha bibi Zainabu (a.s).

Wasomaji wa Quráni wamepewa zawadi katika hafla hiyo, pamoja na waimbaji walioshiriki kwenye program ya (muongozo wa Hussein) kutoka hapa wilayani.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu kupitia matawi yake tofauti, ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kufundisha masomo ya Quráni, na kutengeneza jamii inayofuata mafundisho ya Quráni tukufu na yenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika fani zote za Quráni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: