Sayyid Swafi awakirimu waliofanya wasimamizi wa filamu ya (Ahmadi na mwezi) na amewahimiza kuongeza juhudi

Maoni katika picha
Wasimamizi wa filamu ya (Ahmad na mwezi) inayo fundisha watoto usomaji wa surat Faat-ha, wamekirimiwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Kazi ya utengenezaji wa filamu hiyo imefanywa na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule kwa kushirikiana na wataalamu wa kituo cha Aljuud cha uchoraji wa picha zinazo cheza (katuni) na kituo cha habari katika Atabatu Abbasiyya, nayo ni filamu ya kwanza kutengenezwa kwa ajili ya kufundishia Quráni.

Kikao cha kuwakirimu kimefanywa Ijumaa Alasiri (30 Shawwal 1442h) sawa na tarehe (11 Juni 2021m), Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi aliongea katika kikao hicho, miongoni mwa aliyosema ni: “Tunafurahi sana tunapo ona juhudi za mambo yanayo husu Quráni zinapata maendeleo mazuri siku baada ya siku, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu zifanywe kwa niya ya dhati na kazi yenye kukubalika hususan sisi tuliochini ya kivuli cha Ahlulbait (a.s), katika jambo lisilokua na shaka, kufanya kazi katika maoeneo matakatifu kuna uzuri wake usiopatikana katika maeneo mengine”.

Akaongeza kuwa: “Kuhusu kazi tuliyo ona ya filamu ya (Ahmadi na mwezi), ni kazi nzuri iliyo pangiliwa vizuri sana, mimi nimeangalia mwanzo hadi mwisho na hakika ni kazi yenye mvuto kwa watoto, utaratibu huu yapasa kunufaika nao kwa kuangalia mambo ambayo mwanaadamu anaweza kughafilika nayo”.

Akaendelea kusema: “Baada ya janga la Korona kuna umuhimu wa kuwaita watoto na kuwafundisha, kukutana nao moja kwa moja kuna athari kubwa, hapo mtu anaweza kuonyeshwa sehemu zinazo kosewa moja kwa moja, baada ya kurekebishwa hatarudia kosa tena bali na yeye atageuka mwalimu”.

Akasema: “Jambo zuri ndugu zetu wameanza na surat Faat-ha, naamini matokeo ni mazuri katika kazi hii, faida haiwahusu watoto peke yao bali hadi wakubwa, baadhi ya watu husoma Quráni haraka haraka bila kujali hukumu, hasa katika sura hii tukufu”.

Akakumbusha kuwa: “Hii ni kazi tukufu na imekamilika, aidha inashajihisha kuendelea na mfumo huu katika utoaji wa elimu, hakika picha zinazo cheza (katuni) zinaeleweka haraka”.

Katika kuhitimisha maneno yake Sayyid Swafi akasema: “Katika umuhimu wa kutoa mafunzo ya Akhlaq na maadili mazuri kwa watoto, hakuna yaliyobora kama ufundishaji wa Quráni na mwenendo wa Ahlulbait (a.s) kwenye kufanikisha hilo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: