Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinaendesha mafunzo kwa watumishi wake

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha mafunzo kwa watumishi wake, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuchambua selebasi za masomo.

Mkufunzi wa semina hiyo Dokta Hassan Jadhili amesema: “Sehemu ya kwanza ya mafunzo haya inahusu maelezo ya madhumuni ya selebasi za masomo, kwa kuangazia uhalisia, uwelewa, kanuni na mitazamo”.

Akaongeza kuwa: “Siku zijazo tutaangazia utekelezaji wa wakufunzi kulingana na fani zao na mambo wanayo kubaliana”.

Akaendelea kusema: “Hatua ijayo tutashuhudia uzowefu na vipaji vya wakufunzi katika kuelezea selebasi za masomo, mbele ya walimu wa shule wa Al-Ameed”.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu huandaa semina na warsha mbalimbali kwa watumishi wake kwa lengo la kuwajengea uwezo na kukuza vipaji vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: