Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) imefanya kongamano la kumi na nane

Maoni katika picha: kiongozi wa nadwa
Kituo cha Daru Rasuul (s.a.w.w) chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya kongamano la historia ya Mtume awamu ya kumi na nane kwa njia ya mtandao na kupewa jina la (Mtume mtukufu (s.a.w.w) katika ukamilifu), jioni ya siku ya Ijumaa (29 Shawwal 1442h) sawa na tarehe (11 Juni 2021m).

Nadwa imeongozwa na Dokta Liith Qaabil Waailiy mjumbe wa kituo cha Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w), chini ya ukufunzi wa Shekh Haidari Daakhil Muhammad Ali Abu Swibii, akabainisha tatizo linalo husu historia ya Mtume (s.a.w.w), katika maudhui ya ukamilifu wake, kimaumbile, kinafsi na kimaarifa, tunamshukuru Mwenyezi Mungu alifafanua vizuri na kumtakasa na aibu anazopewa, baadhi ya watu humuona kuwa ni mtu wa kawaida, nadwa imehudhuriwa na wasomi wa historia na wataalamu wa lugha.

Kiongozi wa nadwa amesema kuwa: “Daru Rasuul inavikao vinne kila mwaka, hukutana watafiti wa fani tofauti, hasa fani ya historia na lugha, kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali pamoja na zilizo ibuliwa na wazungumzaji wa kongamano, kongamano la kumi na nane limefanywa chini ya ukufunzi wa Shekh Haidari Dakhil Muhammad Ali Abu Swabii, naye ni mkufunzi wa maarufu wa hauza katika (bahthu khaariji)”.

Akaongeza kuwa: “Haiwezekani kwa kalamu yeyote au ulimi kutofautiana na dalili ya kisheria ambayo waislamu wote wamekubaliana, kongamano lilikuwa na jukumu la kuzikumbusha akili ukweli huo”.

Kumbuka kuwa Daru Rasuul Aádham (s.a.w.w) tangu ilipo anzishwa zaidi ya miaka mitano iliyopita, imefanya miradi mingi ya kielimu inayo lenga jambo moja, nalo ni kuisoma upya historia ya Mtume mtukufu chini ya muongozo wa Quráni na hadithi sahihi, inatumia uwezo wake wote kufuata misingi imara katika kuandika historia hiyo bila kupingana na Quráni tukufu, na kuzingatia kauli ya Mwenyezi Mungu katika surat Qalam isemayo: (Hakika wewe uko juu ya tabia nzuri).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: