Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza tarehe ya kufanyika kongamano la fatwa ya jihadi kifaya awamu ya tano

Maoni katika picha: Ilikuwepo
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza tarehe ya kufanyika kongamano la fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda awamu ya tano, litakalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Uthibitisho wa vyombo vya habari.. ushahidi halisi).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo na makamo rais wa kitengo cha habari katika Ataba tukufu Ustadh Ahmadi Swadiq amesema: “Kongamano litaanza Alkhamisi ijayo (6 Dhulqaadah 1442h) sawa na tarehe (17 Juni 2021m), ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) saa nne asubuhi”.

Akaongeza kuwa: “Kongamano litakuwa na mihadhara mbalimbali pamoja na uwasilishaji wa mada za kitafiti na mashairi, aidha itaonyeshwa filamu ya matukio ya fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda”.

Akasema: “Kongamano litahitimishwa siku hiyo hiyo, kutakuwa na taomko la ufungaji wa kongamano pamoja na maazimio yatakayo andaliwa na wanakongamano”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: