Idara ya Quráni imeratibu safari ya mahafidhu wa Quráni tukufu

Maoni katika picha
Idara ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa safari ya mahafidhu wa Quráni, kama sehemu ya kuwapongeza na kuthamini juhudi yao.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema: “Tunajali sana wasomaji wa Quráni, kila baada ya muda huwa tunafanya jambo la kuonyesha kujali kwetu jambo hilo, huwa tunaandaa safari zenye mafunzo tofauti na mapumziko”.

Akaongeza kuwa: “Kwenye safari hii imetolewa mihadhara mbalimbali inayohusu ulazima wa kushikamana na Quráni tukufu, na umuhimu wa kuihifadhi na kutafakari wakati wa kuisoma”.

Wakina dada waliohifadhi Quráni wameshukuru sana ukarimu wanaofanyiwa na idara.

Kumbuka kuwa idara ya Quráni inalenga kukuza uwezo wa wanawake kitamaduni na kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: