Amepongeza upekee wa tawi: Waziri wa utamaduni ameangalia ushiriki wa Atabatu Abbasiyya katika maonyesho ya vitabu yanayo fanyika Bagdad

Maoni katika picha
Waziri wa utamaduni wa Iraq Ustadh Hassan Naadhim ametembelea tawi la Atabatu Abbasiyya katika maonyesho ya vitabu yanayo fanyika Bagdad awamu ya kumi na nane, chini ya kauli mbiu isemayo: (Kitabu.. na taifa).

Waziri ametembelea korido zinazo wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha utamaduni na elimu na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, ameangalia machapishi mbalimbali ya vitengo hivyo na kusikiliza maelezo kuhusu baadhi ya machapisho hayo.

Waziri amepongeza ushiriki wao na kusema ni wa pekee, akasisitiza kuwa ushiriki huu unafaida kubwa, akasema kuwa alicho kiona ni machapisho mazuri na akawataka waendelee na kazi hiyo tukufu.

Tambua kuwa matawi ya Atabatu Abbasiyya yamekua yakishiriki kwenye maonyesho haya tangu yalipo anzishwa, na wamekua wakitembelewa na vongozi wa Dini na wa kisiasa pamoja na wadau mbalimbali wa elimu na utamaduni, na watu wengine wengi ambao wamesema kuwa hii ni sehemu nzuri ya kupata zawadi za kiroho na kielimu.

Kumbuka kuwa ushiriki wa maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki mwingi uliotangulia, upekee wa machapisho yetu ndio sifa kubwa ya matawi yetu kwenye kila maonyesho, tulikuwa na machapisho tofauti zaidi ya (300), yote yanatokana na kazi ya Ataba tukufu, kuanzia uandishi hadi uchapaji, hiyo ndio sifa ya pekee ya matawi yetu ukilinganisha na matawi mengine, machapisho tunayo onyesha ni kielelezo cha harakati tunazo fanya katika sekta ya utamaduni na elimu pamoja na ubunifu wa watumishi wa Ataba takatifu katika mambo ya utamaduni, elimu na turathi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: