Fatwa ya Marjaa na muitikio wa wairaq: Miaka saba imepita tangu kuokolewa Iraq

Maoni katika picha
Wananchi wa Iraq na wapenda amani duniani kote wanaadhimisha mwaka wa saba tangu ilipotolewa fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda na Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, aliyotoa tarehe kumi na tatu mwezi wa sita mwaka 2014, iliyowataka wairaq wenye uwezo wa kubeba siraha waungane na wanajeshi la serikali kwa ajili ya kuilinda Iraq, raia wake na maeneo matakatifu, dhidi ya magaidi wa Daesh waliokuwa wameteka sehemu kubwa ya mikoa tofauti, wakatishia kuteka mji mkuu Bagdad na mikoa mingine.

Mwitikio wa fatwa hiyo iliyogusa hisia za kila raia wa Iraq ulikuwa wa haraka, watu wa Iraq walijitokeza kwa wingi vijana kwa wazee wakisukumwa na hisia za ubinaadamu katika kupambana na maadui wa Daesh, takwimu rasmi za serikali zinaonyesha kuwa watu waliojisajili walifika milioni tatu na nusu.

Katika vita hiyo yalishuhudiwa mambo ambayo ni vigumu kutokea duniani, wananchi wa Iraq walipigana vita kali sana iliyodumu miaka mitatu na miezi sita, walionyesha ushujaa wa hali ya juu, walitetemesha ardhi chini ya nyayo za madhalimu na maadui, wanaolitakia shari taifa hili, aidha kwenye vita hiyo wamejitolea makumi ya maelfu mashahidi na majeruhi wengi sana, kwa ajili ya kuokoa taifa hili na kulinda maeneo matakatifu.

Hadi Mwenyezi Mungu alipowapa ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, na kutakasa ardhi kutokana na uovu wao pamoja na kuangusha utawala wao, wakaokoa Iraq bali nchi zote za eneo hili na raia wake.

Ushindi huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu haukupatikana ispokua kwa sababu mbili kuu, ambazo ni fatwa tukufu na mwitikio wa wairaq kwa fatwa hiyo.

Kumbuka kuwa tamko la kwanza la fatwa hiyo lilitolewa katika haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) kwenye mimbari ya swala ya Ijumaa kupitia muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, ambaye katika nukta ya nne alisisitiza kuwa:

(Hakika kuwalinda watoto wetu katika jeshi na vikosi vyote vya askari ni jambo tukufu, umuhimu unaongezeka pale inapojulikana kuwa njama za magaidi ni za kidhalimu zikombali na uislamu, hawataki kuishi kwa amani na watu wengine, wanafanya vitendo vya ukatili na umwagaji wa damu na kueneza ubaguzi, sambamba na kupanua uvamizi wao katika mikoa tofauti ya Iraq na nchi jirani, enyi watoto wetu katika taifa la Iraq mnawajibu mkubwa kihistoria, kitaifa na kisheria, jalieni nia yenu ni kulinda taifa la Iraq na umoja wake, na kulinda amani kwa raia wake na maeneo matakatifu na kuondoa wavamizi katika taifa hili.

Wakati ambao Marjaa Dini mkuu anasisitiza kuwa pamoja na nyie, vilevile anawahimiza kupambika na ushujaa msimamo na subira, atakaekufa kwa ajili ya kulinda taifa lake, watu wake na heshima yao atakuwa shahidi –Insha-Allah-… baba na mama wanatakiwa wawahimize watoto wao na mke amhimize mumewe kujitokeza kwenda kulinda taifa na raia wake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: