Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya tamasha la mashairi kuadhimisha kumbukumbu ya kutolewa fatwa kifaya ya kujilinda

Maoni katika picha
Tamasha la usomaji wa mashairi limefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, lililo andaliwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kuadhimisha mwaka wa saba tangu ilipotolewa fatwa ya wajibu kifaya wa kujilinda iliyo hami ardhi ya Iraq na maeneo matakatifu, asubuhi ya leo mwezi (2 Dhulqaadah 1442h) sawa na tarehe (13 Juni 2021m).

Mkuu wa mkoa wa Karbala amehudhuria kwenye tamasha hilo pamoja na viongozi wa jeshi na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na makamo wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya uongozi na wakuu wa vitengo bila kuwasahau viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na watumishi wengine.

Tamasha limefunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa la Iraq na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa).

Baada ya hapo ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ukawasilishwa na rais wa kitengo cha Dini Shekh Swalahu Karbalai, akabainisha kuwa: “Katika siku kama ya leo miaka saba iliyo pita, Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu alitoa fatwa tukufu ya jihadi kifaya ya kujilinda, ambayo iliitikiwa kwa wingi na wananchi wa Iraq na kuwa sababu ya kuwashinda magaidi wa Daesh, na kuandika historia kubwa ya utii wao kwa Marjaa Dini mkuu na kuonyesha ushujaa wa hali ya juu katika kupigania taifa hili na maeneo matakatifu, hadi damu tukufu za mashahidi zikafanikiwa kuleta ushindi, tunamuomba Mwenyezi Mungu ailinde Iraq na awarehemu mashahidi na kuwaponya haraka majeruhi”.

Ukafuata ujumbe kutoka kwa mkuu wa mkoa Ustadh Naswifu Jaasim Khatwaabi, akasema kuwa: “Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani amewalinda wairaq kwa utukufu wa joho lake takatifu, fatwa aliyotoa ni fahari kwa wairaq wote, ni fatwa dhidi ya batili na umwagaji wa damu kwa ubaguzi, nayo ni ujumbe wa Ahlubait Rasuul (s.a.w.w) dhidi ya makundi ya kigaidi yanayo eneza ufisadi duniani, fatwa hiyo imekuja kuwamaliza magaidi chini ya umoja wa raia wa Iraq katika kutii fatwa”.

Akabainisha kuwa: “Tangu kuanzishwa kwa kikosi cha Abbasi (a.s) kimefanya kazi bega kwa bega na jeshi la serikali, na kimeleta ushindi mkubwa sambamba na kujitolea mashahidi wengi, pongezi kubwa ziwaendee familia za mashahidi na majeruhi kwa ushujaa wao wa kulinda taifa la Iraq”.

Wakaanza kupanda jukwaa washairi mbalimbali waliosoma mashairi ya aina tofauti, yaliyotaja ushujaa wa wapiganaji na ushindi wa jeshi na raia wa Iraq, na jinsi walivyo itikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kulinda taifa la Iraq na maeneo yake matakatifu.

Tamasha likahitimishwa kwa kuwapa zawadi washairi, kisha wahudhuriaji wakaelekea kwenye maonyesho ya picha zinazo onyesha kazi kubwa iliyofanywa na kikosi cha Abbasi (a.s) katika vita ya ukombozi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: