Balozi wa Misri nchini Iraq amepongeza machapisho ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kielimu na kitamaduni

Maoni katika picha
Balozi wa Misri nchini Iraq Waliid Ismaili amepongeza machapisho yaliyopo katika tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa mjini Bagdad, chini ya kauli mbiu isemayo: (kitabu.. na taifa), machapisho waliyo nayo yanaakisi harakati zinazo fanywa na Ataba tukufu katika sekta ya elimu na utamaduni hapa Iraq.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea korido ya Atabatu Abbasiyya inayo wakilishwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, amezunguka katika korido hizo na kusikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa vitengo vivyo wanaoshiriki maonyesho hayo, waliofafanua baadhi ya vitabu walivyo navyo, vilivyo pelekea aseme kuwa Atabatu Abbasiyya inamchango mkubwa katika sekta ya uandishi wa vitabu na usambazaji.

Kumbuka kuwa ushiriki wa maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki mwingine mwingi uliotangulia, upekee ni sifa kubwa tuliyonayo kwenye maonyesho kama haya, tuna aina zaidi ya (300) za machapisho tofauti, yametokana na kazi halisi ya Ataba tukufu, kuanzia uandishi hadi uchapishaji, huo ndio upekee wa tawi letu na matawi mengine yanayo shiriki, vitabu na machapisho mbalimbali tuliyo nayo ni kielelezo kikubwa cha kazi inayofanywa na Ataba tukufu katika sekta ya utamaduni, elimu na turathi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: