Ukumbi wa haram ya Abbasi imetandikwa miswala mipya

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Maasumah (a.s), ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umetandikwa miswala mipya ya kifahari.

Makamo rais wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutandika miswala na kuibadilisha hufanywa kila wakati kwa kufuata ratiba maalum, au kulingana na mahitaji hasa unapotokea uharibifu katika mswala, usiku wa jana mwezi pili Dhulqaadah watumishi wa kitengo chetu kwa kushirikiana na watumishi wa idara ya miswala na usimamizi wa haram pamoja na waliojitolea kutoka vitengo vingine wametandika miswala mipya elfu moja yenye rangi nzuri, ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inayo endana na utukufu wa eneo hili”.

Akaongeza: Kazi ya kutandika miswala ilitanguliwa na kutandua miswala ya zamani na kwenda kuiosha pamoja na kupiga deki na kupuliza dawa sambamba na kubaini sehemu za kutandika miswala kwa kuzingatia ukubwa wa kila sehemu, ndipo ikatandikwa kwa kuzingatia ukubwa na mapambo yake.

Kumbuka kuwa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu kinamajukumu mengi, miongoni mwa majukumu yake ni kutandika miswala na kuisafisha kila baada ya muda fulani, kwa ajili ya kulinda uzuri wa haram tukufu na kudumisha hali nzuri ya kiroho anayopata mtu anayekuja kufanya ziara katika haram tukudu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: