Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza kwa shindano la kutengeneza filamu fupi

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya ofisi ya katibu mkuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetandaza kuanza kwa shindano la utengenezaji wa filamu fupi hapa Iraq, washiriki wote watapewa vyeti vya ushiriki pamoja na zawadi za mali.

Shindano linamaudhui zifuatazo:

  • 1- Umuhimu wa vitendo vizuri.
  • 2- Maadili meme.
  • 3- Mila zinazo ingizwa katika jamii yetu.
  • 4- Changamoto za kinafsi na njia za kuzitatua.
  • 5- Nafasi ya mwanamke mwenye kujiheshimu.
  • 6- Maendeleo mema.
  • 7- Uwelewa wa afya.

Makundi yanayo shiriki shindano hili ni:

Kwanza: Watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Pili: Watengenezaji wote wa filamu fupi hapa Iraq.

Mshiriki anahiyari ya kuchagua maudhui anayotaka katika hizo zilizotajwa hapo juu, kazi zote zinatakiwa kutimiza vigezo vilivyo tajwa na kamati ya wataalamu.

Kumbuka: Matokeo yatakayo tolewa na kamati ndio ya mwisho.

Zawadi zitategemea kikosi ulicho shiriki pamoja na kueleweka kwa maudhui uliyo chagua.

Zawadi zitakuwa kama zifuatavyo:

  • 1- Kikosi cha mbio: washindi watatu wa mwanzo watapewa vyeti na zawadi za mali:

Mshindi wa kwanza: milioni moja na laki tano dinari za Iraq (1,500,000).

Mshindi wa pili: milioni moja dinari za Iraq (1,000,000).

Mshindi wa tatu: laki saba na elfu hamsini dinari za Iraq (750,000).

  • 2- Kikosi cha mieleka: washindi watatu wa mwanzo watapewa vyeti vya ushiriki na zawadi za mali.

Mshindi wa kwanza: laki saba na elfu hamsini dinari za Iraq (750,000).

Mshindi wa pili: laki tano dinari za Iraq (500,000).

Mshindi wa tatu: laki mbili na elfu hamsini dinari za Iraq (250,000).

Filamu tano bora za mieleka zitapewa zawadi kwa ajili ya kuwashajihisha waweze kushiriki kwenye mashindano makubwa, na watapewa dinari za Iraq laki mbili (200,000).

Kumbuka masharti ya shindano ni:

  • 1- Filamu haitakiwi kuzidi dakika tano.
  • 2- Mshiriki anatakiwa kuchagua maudhui moja miongoni mwa maudhui zilizo tajwa.
  • 3- Kazi isiwe imeshawahi kuonyeshwa na mtu yeyote au kushiriki kwenye shindano lingine au ipo kwenye intanet.
  • 4- Unazingatiwa ujumbe uliopo kwenye kazi, na uwe na vyanzo sahihi.
  • 5- Kazi itengenezwe kwa lugha ya kiarabu au lugha nyingine yeyote, kwa sharti itafsiriwe kwa lugha ya kiarabu.
  • 6- Muhusika wa kazi awe ndio mmiliki wa haki zote, na awe na haki ya kukabidhi kazi na vitu vinavyo hitajika kwenye shindano.
  • 7- Filamu isihusike na kutangaza biashara yeyote au kuwa na nembo ya kibiashara.
  • 8- Kazi iwekwe kwenya cd au (flashi) na ikabidhiwe kwenye kitengo cha maendeleo endelevu katika Ataba tukufu, au itumwe kwa barua pepe kwenye anuani ifuatayo (documentaries@alkafeel.net).
  • 9- Kazi zianze kukabidhiwa mwezi (1 Dhulqaadah 1442h) hadi mwezi (5 Dhulhijjah 1442h)
  • 10- Atabatu Abbasiyya tukufu itakuwa na haki ya kutumia kazi hizo kwa namna itakavyo na mtengenezaji hatakuwa na haki yeyote baada ya kukabidhi kazi yake akishinda au asishinde.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: