Kuhitimisha sehemu ya kwanza ya program ya kujenga uwezo wa kiidara

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kimemaliza sehemu ya kwanza ya semina ya kujenga uwezo wa mambo ya kiidara kwa marais wa vitengo na viongozi wengine katika Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo husu uboreshaji endelevu na utatuzi wa changamoto na uchukuaji wa maamuzi.

Kukamilika kwa semina hiyo kumehusisha ufanyaji wa mtihani ndani ya moja ya kumbi za chuo kikuu cha Al-Ameed na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na makamo katibu wake mkuu pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi.

Rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Hassan Jaabir ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na vigezo vya kielimu katika ufundishaji, leo tumetoa mtiani maalum kufuatia masomo yaliyo fundishwa katika semina hii, yanayolenga kujenga uwezo wa mambo ya kiutawala kwa viongozi hawa, zitafuata semina zingine hadi tumalize vipengele vyote vya masomo haya”.

Akaongeza kuwa: “Semina hizi zinatokana na mtazamo wa uongozi mkuu wa Ataba tukufu chini ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi na katibu wake mkuu, walio ona umuhimu wa kujifunza nadhariya za kisasa katika uongozi na kuzifanyia kazi, ili kuiwezesha Atabatu Abbasiyya tukufu kufanya kazi kitaasisi katika maeneo yote”.

Akabainisha kuwa: “Program hii inaendeshwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, chini ya wakufunzi walio bobea, mafunzo yanatolewa kwa hatua mbalimbali, hatua ya kwanza imelenga marais na wakuu wa idara, itafuata hatua nyingine itakayo lenga viongozi wa ofiri, tutahakikisha kila mtumishi anafamu wajibu wake kiutendaji, jambo hili litasaidia kuweka nidhamu kati ya viongozi na watumishi wa kawaida, na hatimae kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi na ndugu yake Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: