Kuanza awamu ya tano ya kongamano la fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Alkhamisi ya mwezi sita Dhulqaadah (1442h) sawa na tarehe (17 Juni 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), shughuli za kongamano la awamu ya tano la fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda zilianza chini ya kauli mbiu isemayo: (uthibitisho wa habari.. ni ushahidi hai).

Hafla ya ufunguzi imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu pamoja na naibu wake na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo bila kuwasahau wakuu wa idara, na wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala na viongozi wa Dini, wakisiasa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Kongamano limefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyosomwa na msomaji wa Ataba mbili bwana Haidari Jalukhani, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, halafu ukasomwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), ukafuata ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, halafu mshairi bwana Najaahu Arsaani akasoma shairi lililoburudisha masikio ya wahudhuriaji.

Kisha ikaonyeshwa filamu maalum ya matukio ya fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda, iliyo andaliwa na kikosi cha Atabatu Abbasiyya kutokana na kitabu chenye juzuu (62) kinacho eleza fatwa hiyo takatifu na yaliyojiri baada ya fatwa hadi kupata ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh.

Baada ya hapo ikasomwa mada ya kitafiti iitwayo (kitabu cha fatwa kifaya ya kujilinda juzuu la tatu utafiti kuhusu umuhimu na madhumuni) iliyo wasilishwa na Dokta Mikdadi Fayaadh.

Nimatarajio yetu jioni ya leo vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti vitaendelea hadi mwisho, kongamano litapambwa na hafla ya mashairi itakayo fanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya washairi walio bobea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: