Sayyid Swafi: Mlango wa kitabu cha fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda uko wazi kupokea kila kitu ambacho hakija andikwa au kutajwa

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa: Mausua (kitabu) cha fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda uko wazi kuandika taarifa zote za ushujaa wa watu walioitikia fatwa hiyo tukufu na kuchapishwa katika matoleo yajayo.

Ameyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda, lililofanywa siku ya Alkhamisi mwezi sita Dhulqaadah (1442h) sawa na tarehe (17 Juni 2021m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Uthibitisho wa habari.. ni ushahidi hai).

Lifuatalo ni tamko lake kuhusu swala hilo:

Fatwa hii tukufu ni jambo muhimu lazima lifundishwe, sisi katika Atabatu Abbasiyya baada ya kuona kuna tatizo la kutunza taarifa za matukio yetu, mambo mengi yanafanyika na kupita bila kuandikwa na kutunzwa na tunapotaka kuwakumbuka hujikuta mengi tumesha yasahau kana kwamba hayakutokea, hivyo vizazi vijavyo kutojua mambo yaliyotokea kwa sababu hayajaandikwa, ndipo tukaona umuhimu wa swala hili, kuandikwa tena kwa mikono ya wairaq wenyewe, ninawaomba ndugu zangu wajitahidi kuandika taarifa za kila aliyeshiriki kwenye vita hii takatifu, kuna kamati nyingi zinazo simamia swala hilo.

Baadhi waliitika wengine wakawa kati kwa kati na wengine hawakuitika, mlango bado uko wazi kwa kila mwenye kitu ambacho hakijatajwa au kuandikwa atuletee, ni wajibu wa ndugu zetu kuandika kila kitu kiwe cha ushindi au kushidwa, tutahakikisha kinaingizwa katika kitabu hiki chenye juzuu (62), tunatarajia kiongezwe makumi ya majuzuu zingine, tayali ndugu zetu wamesha anza kukusanya taarifa zitakazo ongezwa, na baadhi ya mambo ambayo hayakuwepo, lazima tuandike mambo yetu kwa utaratibu unaokubalika, aidha kitabu hiki kitakuwa wazi kufanyiwa masahihisho ya kielimu na kila atakayetaka kufanya hivyo, kama kilivyo wazi kwa kila anayetaka kusoma historia ya jambo hili, tusiache kusaidia katika jambo hili, tumefanya tulicho weza, hatua ya kwanza lazima ufundishwe ukweli huu kuhusu fatwa takatifu, utakumbukwa kila wakati kwa sababu ni matukio ya kweli.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: