Swali linahitaji jawabu: Kwanini Iraq ilivamiwa na Daesh? Tatizo ni nini? Tunauhakika gani kama jambo hili halitarudia tena?

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ameuliza maswali mengi yanayo hitaji majibu, kuhusu sababu za magaidi wa Daesh kuvamia Iraq, yafuatayo ni sehemu ya maswali hayo:

Kwanini Iraq ilivamiwa? Tatizo lilikuwa nini? Hadi magaidi hao wakaweza kuteka mji mkubwa na wakaendelea kuteka miji mingine, nini tatizo? Tunauhakika gani kama hali hiyo haitajirudia? Kujibu maswali haya kunahitaji ujasiri na uwazi, kwa sababu hilo ni tatizo kubwa sana, fatwa ikawa ni jambo tukufu mno, ikaja kuzuwia njama mbaya, lakini kwa nini mambo haya yalitokea, tatizo ni mfumo wa kisiasa? Au tatizo ni jeshi? Au ufisadi uliokithiri katika taifa? Au tatizo ni kuwapa madaraka watu wasiokuwa na sifa wala uwezo wa kuongoza taifa? Tatizo liko wapi?!! Lililo tokea ni jambo hatari sana halijawahi kutokea katika nchi zingine duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: