Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya ametaja mambo muhimu yaliyo fanikishwa na fatwa tukufu ya jihadi kifaya ya kujilinda, katika ujumbe aliotowa wakati wa ufunguzi wa kongamano la fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda, miongoni mwa aliyosema ni:
Fatwa tukufu imelinda taifa, wananchi, maeneo matakatifu na heshima, aidha imezuwia genge la kigaidi la Daesh kukaa hapa Iraq, mnajua wazi kuwa historia inaweza kupotoshwa, kama inavyo weza kuandikwa kwa usahihi pia inaweza kuandikwa kwa kupotoshwa.
Fatwa inapokuwa na umuhimu huu mkubwa wa kulinda taifa na kuzuwia njama mbaya, pamoja na kuzuwia kuenea kwa magaidi hadi katika nchi zingine, hili ni jambo kubwa, wasomi wafanye uchunguzi ilikuwa vipi likaanzishwa genge la magaidi, nani alikuwa nyuma yake? Alikuwa anataka nini?! Hadi ikalazimika kutolewa fatwa hii tukufu iliyobadilisha matokea na kutibua njama zao.