Kuhitimisha kongamano la fatwa kifaya takatifu ya kujilinda

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu Alkhamisi ya leo mwezi sita Dhulqaadah (1442h) sawa na tarehe (17 Juni 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) imekamilisha awamu ya tato ya kongamano la fatwa kifaya ya kijilinda, lililofanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Uthibitisho wa habari.. ni ushahidi hai).

Katika hafla ya kufunga kongamano hilo yamesomwa maazimio yaliyo andaliwa na kamati ya maandalizi pamoja na kamati ya taaluma, na kusomwa na Dokta Mushtaqu Abbasi Muan, yafuatayo ni maazimio hayo:

Kwanza: Mlango wa kupokea taarifa, shuhuda, visa na kila kinacho husiana na matukio ya utekelezaji wa fatwa takatifu ya jihadi kifaya kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa mojo, uko wazi kwa ajili ya kuziandika na kuzitunza kwenye kitabu (mausua).

Pili: Kutafsiri kitabu (mausua) katika lugha zingine kidogo kidogo kulingana na mazingira, ili kuijulisha dunia ushujaa wa watu walio itikia wito wa Marjaa Dini mkuu.

Tatu: Kufungua kituo kitakacho husika na mambo yanayo husiana na fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda, na yanayo fungama nayo kama turathi, ili kutunza historia ya umma na mafanikio yake.

Nne: Kubuni mkakati wa kihabari utakao lenga kufikisha ujumbe uliomo kwenye kitabu (mausua) kwa makundi tofauti ya watu, ili kusambaza ujumbe huo kwa njia bora, kwa kushirikiana kati ya kitengo cha habari na jumuiya ya taaluma Al-Ameed.

Tano: Watafiti na wanafunzi wa masomo ya juu waendelee kuandika mambo yanayo husu uitikiaji wa mwito wa Marjaa, na kufichua siri zake na hazina zake, kituo tulicho shauri kuanzishwa kwake (katika azimia la tatu) kiwajibike kusaidia jambo hilo, ili kuwa na vyanzo vingi vinavyo elezea jambo hilo.

Sita: Kutumia vyanzo sahihi kielimu kwa kila jambo linalo husu kitu kilichotokea katika utekelezaji wa fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda, pamoja na yatokanayo na mambo hayo kama vile kuunda vikosi mbalimbali, kutoa elimu, kuunda kanuni za kisheria au kiserikali.

Saba: Kutoa maoni ya kuelezea ushujaa wa watu walioitikia fatwa katika selebasi za masomo, hususan inapozungumziwa historia ya sasa, kitabu hiki (mausua) kiwe msingi wa somo hilo.

Nane: Kufanya mashindano ya kibunifu (mashairi, visa vifupi, maigizo) yaliyo simamishwa katika awamu iliyopita kwa sababu ya janga la Korona, mkakati huo unasaidia utunzaji wa taarifa.

Tisa: Kuchapisha mada za kitafiti zilizo tolewa kwenye makongamano haya yaliyo fanyika miaka ya nyuma.

Baada ya hapo zawadi zikatolewa kwa kikosi cha watu wanaofanya shughuli za kukusanya na kuandika kitabu (mausua) ya fatwa takatifu ya jihadi kifaya pamoja na vyombo vya habari vinavyo saidia kuonyesha matukio hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: