Ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Alkhamisi mwezi sita Dhulqaadah (1442h) sawa na tarehe (17 Juni 2021m), kimefanyika kikao cha usomaji wa mashairi, kikao hicho ni sehemu ya kongamano la awamu ta tano katika makongamano la fatwa takatifu ya jihadi kifaya ya kujilinda, lililofanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Uthibitisho wa habari.. ni ushahidi hai).
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano Sayyid Aqiil Abdulhusein Yaasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kamati ya maandalizi ilikipa umuhimu kikao cha usomaji wa mashairi kutokana na umuhimu wake wakati wa vita dhidi ya makaidi wa Daesh, mashairi yalikuwa na nafasi kubwa ya kuamsha hisia za wapiganaji na kueleza ushujaa wao kwa watu, ukizingatia kuwa ni fani inayokubalika na wairaq wengi”.
Akaongeza kuwa: “Wameshiriki wasomaji mashuhuri wa mashairi, akiwemo Muhamammad Faatwimi kutoka mkoa wa Baabil, Haidari Shibani kutoka Najafu, Ali Swafrani kutoka mkoa wa Muthanna, washairi wa Karbala walioshiriki ni: Ali Zubaidi na Zainul-Aabidina Saidi na Hamza Samawi”.
Washairi walioshiriki usomaji wa mashairi, wameshukuru na kupongeza kamati ya maandalizi ya kongamano kwa kuwapa fursa ya kusoma mashairi yao katika sehemu hii takatifu, katika kuadhimisha fatwa tukufu na ushujaa wa watu walioitikia fatwa hiyo.