Maktaba ya Ummul-Banina imeanza msimu wa tatu wa warsha ya kielimu ya kuhakiki nakala kale

Maoni katika picha
Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza msimu wa tatu wa warsha ya kielimu inayo endeshwa kwa njia ya mtandao chini ya kauli mbiu isemayo: (Utamaduni katika uboreshaji endelevu) warsha ya kielimu kuhusu uhakiki wa nakala-kale.

Mkuu wa maktaba bibi Asmaa Raád Al-Abaadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Awamu ya tatu ya warsha ya kielimu inahusu fani za maktaba, na tunaanza na uhakiki wa nakala-kale, ikiwa ni pamoja na kutoa utambulisho wa nakala-kale, na namna zilivyofika mikononi mwetu pamoja na umuhimu wake, na vituo vikubwa vya kimataifa vinavyo tunza nakala kale, sambamba na kuangalia idadi, majina na njia za uhakiki wake, na mambo mengine muhimu katika sekta hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Wawezeshaji wa warsha walikua ni Dokta Imani Swalehe Mahadi rais wa kitengo cha nakala-kale katika kituo cha Ihyaa Turathi Ilmiy Al-Arabiy, Dokta Nahadi Ni’mah Hassan mtendaji wa kitengo cha historia/ kitivo cha malezi katika chuo kikuu cha Bagdad, wamezungumza mada tofauti zinazo endana na anuani ya warsha”.

Akasema: “Warsha imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wasomi wa maktaba na wahakiki wa nakala-kale, kulikua na michango na maoni yaliyo changamsha warsha na kuifanya kuwa hai”.

Akamaliza kwa kusema: “Uhakiki wa turathi unahusisha mambo mengi yenye uhusiano katika maisha, yanayoweza kuwa msingi wa kutengeneza jamii, umma hautakiwi kutosheka na maarifa yaliyowafikia, bali kuyaboresha na kuandaa kwa ajili ya vizazi vijavyo, hiyo ndio kazi tunayofanya kwa bidii zote katika maktaba ya Ummul-Banina ya wanawake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: